Duration 9:38

TUNAOMBEA AMANI TANZANIA

873 watched
0
6
Published 7 Mar 2020

Watanzania tunaitaka katiba Mpya yenye maoni yetu jinsi tunavyotaka kuongozwa. Katiba ya zamani ni ya Chama tawala CCM na wanaitumia kututawala tusivyopenda. Tunataka katiba Mpya Sasa na kama Siyo Sasa tunaitaka Sasa hivi. Ni katiba Mpya ndiyo itakazuia chama cha kisiasa kutumia dola kutisha vyama vingine ili Kibaki madarakani. Dola Siyo Mali ya chama cha kisiasa Dola ni mali ya watanzania na haifai kutumiwa kulinda chama tawala. CCM kutumia DOLA ili wabaki madarakani ni Makosa makubwa. Hii itavifanya vyama vya kisiasa Tanzania vitafute DOLA yenye zana za kivita ili kupambana na DOLA ya CCM na hiyo itakuwa Siasa ya kutumia silaha za kivita badala ya Siasa ya ushawishi wa Maneno. Kama watumishi wa Mungu hatutaki Siasa za Tanzania zifanywe kwa kutumia DOLA kwani itamaanisha siasa ni vita wakati jukumu letu ni kuwaombea wenye mamlalaka tuushi kwa amani. 1 Timotheo 2:1-3 [1]Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; [2]kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. [3]Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ILI TANZANIA TUWE NA AMANI LAZIMA TUWE NA KATIBA MPYA INAYOTENGANISHA DOLA NA VYAMA VYA SIASA ILI CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA KISITUMIE DOLA KUTISHA VYAMA VINGINE ILI KIBAKI MADARAKANI. Tunasema mjadala kuhusu katiba Mpya Siyo kiporo kilichochacha, bali hatuwezi kuwa na uchaguzi huru bila katiba Mpya kwani Chama tawala kitatumia DOLA kubaki madarakani badala ya kura. TIZAMA VIDEO USIKIE AUDIO YAKE

Category

Show more

Comments - 1