Duration 9:13

Sheikh Issa Ponda: Msimamo wa Kupinga Dhuluma ni Msimamo Niliokulia Nao Tangu Utotoni

250 watched
0
3
Published 25 Nov 2021

Moja kati ya sauti muhimu sana katika harakati za kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini Tanzania ni Katibu wa Shura ya Maimamu nchini Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye amekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya kujenga Tanzania ya haki na inayopinga dhuluma za aina zote. Sheikh Ponda amekuwa akijihusisha na harakati hizi kwa miaka mingi, muda mwengine kwa gharama kubwa ya usalama na ustawi wake kama Mtanzania, akijikuta kwenye mivutano ya mara kwa mara na vyombo ulinzi na usalama vya Tanzania. The Chanzo ilimtembelea Sheikh Ponda ofisini kwake Ilala, Dar es Salaam, ili kufanya naye mazungumzo kuhusiana na maisha yake ya uongozi wa kidini na uanaharakati wake. Kwenye mazungumzo hayo ya takriban saa moja, Sheikh Ponda amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake pamoja na muelekeo wa Tanzania kama nchi kijamii, kisiasa na kiuchumi. Kwenye sehemu hii ya kwanza ya mahojiano haya, Sheikh Ponda anaeleza, pamoja na mambo mengine, jinsi maisha yake binafsi yalivyofungamana na mapambano dhidi ya dhuluma tangu kipindi cha toto wake na jinsi ambavyo hawezi kuishi maisha mengine ukiachana na hayo. #TheChanzo

Category

Show more

Comments - 0