Duration 1:23:43

ROHO ZIZUIAZO MATOKEO (IV) - PASTOR SUNBELLA KYANDO

11 056 watched
0
126
Published 31 May 2021

Sio kila ambaye anazuia matokeo yako ni lazima atoke mbali,mara nyingi shetani hutumia watu walio karibu na wewe sana.Wakati Samweli ametumwa na Mungu kwenda kumpaka mafuta ya kuwa mfalme mtoto mmoja wa Yese,Yese mwenyewe hakumuhesabu Daudi kama anaweza kuwa mfalme.Baba yake mzazi ndio alikuwa wa kwanza kutaka kukwamisha safari ya Daudi ya kuelekea kwenye ufalme.Na hata baada ya Daudi kupakwa mafuta bado aliendelea na kazi aliyokuwa anafanya(kuchunga mifugo ya baba yake).Sio lazima Mungu akisema kitu na wewe uanze kuona matokeo hapohapo,siku zote Mungu hufanya kazi kwa majira sahihi. Sauli alikataliwa na Mungu lakini hakutoka kwenye ufalme siku ileile na Daudi alipakwa mafuta ya kuwa mfalme lakini hakuwa mfalme siku ileile.Kwa kuwa tu unapotaka kufika unaona kuna watu tayari tena wenye majina makubwa haina maana kuwa nafasi yako haipo.Wanaweza wakawepo lakini Mungu akawa ameshawakataa.Majira yakifika ya Mungu kukuinua atatengeneza mazingira ya wewe kufika pale alipokuitia,atawatoa wengine na wewe atakuketisha. Endelea kushikilia neno ambalo Mungu amelitamka kwako, haijalishi mazingira yanapinga,Yeye aliyesema atathibitisha. UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322 Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii Like our Facebook: https://www.facebook.com/Therealityof ... Follow our Instagram: https://www.instagram.com/realityofch ... Subscribe our YouTube: /channel/UC67L ... Also Subscribe Roc worshippers youtube channel:/channel/UCyVhAzjcFaJH7lxgiMQviGQ

Category

Show more

Comments - 20