Duration 1:37

BREAKINGNEWS LISSU KUREJEA TANZANIA SIJI KUJIFUNGIA NDANI

7 089 watched
0
42
Published 1 Jul 2021

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema chama hicho kikitengeneza utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kudai katiba mpya, atarejea nchini. Lissu ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, tarehe 1 Julai 2021, akizungumza kwa njia ya mtandao, katika uzinduzi wa kongamano la kudai katiba mpya, lililofanyika kwenye ukumbi wa Baracuda, Tabata jijini Dar es Salaam. Mwanaaiasa huyo aliyeko nchini Ubelgiji, amesema chama hicho kikitaka katiba mpya ipatikane, lazima kishirikishe wananchi. " Tuwaandae wananchi kwenye mikutano ya hadhara na mimi niwaahidi tukitengeneza utaratibu wa mikutano ya hadhara, nakuja Tanzania. Nitakuja Tanzania kufanya mikutano ya hadhara, sio kuja kujifungia chumbani na kukaa kwenye vikao vya ndani. Tujiandae kwenda kwa wananchi tutapata katiba mpya," amesema Lissu. 🔘JE, NA WEWE UNA HABARI? 🔘WASILIANA NA MwanaHALISI TV ( +255 767 400402), 🔘WhatsApp ( +255 692 318213) 🔘Email: mwanahalisitvnews@gmail.com 🔘KWA HABARI ZA KILA SIKU: http://mwanahalisionline.com

Category

Show more

Comments - 13