Duration 44:10

LIVE: MAALIM SEIF AVUNJA UKIMYA MBOWE KUSHAMBILIWA/ATAJA VIKWAZO 10 UCHAGUZI 2020

33 659 watched
0
173
Published 10 Jun 2020

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimebainisha vikwazo kumi vitakavyosababisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 kutokuwa huru, haki na unaoweza kuacha majeraha kwa Watanzania. Vikwazo hivyo, vimebainishwa leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020 na Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Maalim Seif amesema, “Tunahitaji kuwa na uchaguzi utakaowaacha Watanzania wakiwa na furaha na matumaini baada ya kutekeleza haki na wajibu wao wa kidemokrasia wa kuchagua viongozi wanaowataka.”Amesema, kwa bahati mbaya, ikiwa imesalia miezi miwili tu kuelekea kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu, mazingira ya kisiasa nchini hayatoi taswira ya uchaguzi unaoweza kuiacha nchi yetu salama.

Category

Show more

Comments - 161