Duration 7:46

HATIMA YA GWAJIMA, POLE NA JERRY SILAA KUITWA KAMA KUU KUANZIA SASA

205 watched
0
1
Published 18 Dec 2021

WABUNGE watatu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Jerry Silaa (Ukonga), Josephat Gwajima (Kawe) na Humphrey Polepole (Kuteuliwa) hatma ya adhabu yao ipo chini ya Kamati Kuu ya Chama hicho itakapowaita wakati wowote kuanzia sasa. Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama hicho, Shaka Hamdu Shaka, baada ya kuamalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa CCM, Mh Samia Suluhu Hassan, amesema maamuzi ya wanachama hao inategemea hekima ya kikao. Shaka amezungumzia kuhusu maandalizi ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM ambapo maandalizi ya sherehe hizo yatazinduliwa rasmi Januari 29 Mwaka 2022 Zanzibar Mkoa wa kusini Unguja. Katika hatua nyingine Kamati hiyo imempongeza Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwakusimamaia vyema ilani ya CCM. Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa imekutana Desemba 18, 2021 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 toleo la Mwaka 2020 ibara ya 108kifungu Cha pili. USISAHAU KU SUBSCRIBE CHANNEL YETU ILI UWE UNAPATA UPDATE MPYA KILA TUNAPO WEKA HABARI MPYA WAKATI WOWOTE BONYEZA HAPA CHINI KWENYE MAANDISHI YA BLUU /channel/UCcCo ... https://www.instagram.com/kahamatvonline/ #KAHAMATVONLINE #HABARIZAHIVIPUNDE

Category

Show more

Comments - 0