Duration 38:40

MFADHILI MTANZANIA: Safari ya kutembelea watoto - Kijiji cha Mkombozi-Mtera-Dodoma. 07&.

43 watched
0
2
Published 3 Sep 2021

MFADHILI MTANZANIA ni mradi (project) wa kusaidia watoto/wanafunzi hasa waliotoka katika mazingira magumu kwa kufiwa na mzazi/wazazi wao (yatima). Mradi huu umeasisiwa na mchungaji ANYELWISYE JONAS wa kanisa la PHAMT Usharika wa Bethlehem uliopo Kikuyu Dodoma - Tanzania. MALENGO Mfadhili Mtanzania ni mradi unaolenga mambo makuu matatu. Ambazo ni: 1. Kumfadhili Mtanzania anayeishi katika mazingira magumu, ili kumjengea uwezo wa kujikwamua kutoka katika mazingira hayo na kuwa na maisha bora. 2. Kuhamasisha Watanzania kuwa wafadhili wa ndugu zao Watanzania wanaoishi kwenye mazingira magumu. 3. Kutoa elimu ya afya na ujasiriamali kwa watoto/vijana waliopo masomoni na waliopo mtaani. Mpaka sasa watoto 32 wa shule za msingi na sekondari wenye mahitaji hayo (ya muhimu) wameshahudumiwa kuanzia mwaka 2019, 2020, hata sasa 2021 kwa kupewa mavazi (sare za shule, nguo za kushindia, taulo za kike (pads), mashuka, n.k), madaftari, kalamu, pia na bima ya afya. Na wanaofadhili ni wale wote wenye kupenda kutoa sadaka zao za misaada kwa watoto kama hawa kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha au kutoa huduma kama zilivyoorodheshwahapo juu. Watoto wanaoendelea kuhudumiwa ni kutoka maeneo ya Mtera na sasa tumepanua huduma hii kwa kuwafikia na watoto wengine katika maeneo mengine ndani ya mkoa wa Dodoma; lengo ni kuwafikia watoto 100 mwishoni mwa mwaka huu 2021 na baadaye kuwafikia watoto nchi nzima. Ili kuweza kuwafikia watoto hawa kwa sadaka yako (msaada), wasiliana nasi Kwa namba hizi za simu: +255 714 007 393 au/na +255 689 299 680 Kwa email 📧: mfadhilimtanzania@gmail.com Na MUNGU WA MBINGU NA NCHI AKUBARIKI /AWABARIKI SANA.

Category

Show more

Comments - 4