Ester William Mollel ni mama anayeishi na mtoto wa miaka 10 aliyeanza kuugua tangu akiwa na miezi sita. Kulingana na madaktari mtoto Ibrahimu alipata hitilafu ya ubongo wa nyuma wakati akizaliwa. Ester anaishi kwa kutegemea misaada ya watu.Mwandishi wetu wa Arusha Veronica Natalis amemtembelea nyumbani kwake. #kurunzi