Duration 3:22

WATU WASIO JULIKANA WAUA BABA, MAMA, NA MTOTO KIKATILI WANASWAKA NA POLISI.

1 084 watched
0
7
Published 19 May 2021

KIGOMA. JESHI la Polisi Mkoani Kigoma Limethibitisha Kutokea vifo vya watu watatu wa familia moja baada ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wakiwa wamelala katika kibanda shambani wakifanya uangalizi wa mazao. Kamanda wa Polis mkoa wa Kigoma James Manyama amesema Tukio hilo limetokea Tarehe 18 May mwaka huu, katika kijiji cha Kazuramihunda kata ya Kasanda Wilayani Kakonko mkoani Kigoma. Amesema umauti umemkuta Baba wa familia Bw. Masabile Kamana mwenye umri wa miaka 58 muha, na Mke wake Debora Masabila Raia wa Burundi anayekadiliwa kuwa na miaka 36-42 na Mtoto wao aitwaye Neila Masabila mwenye umri wa miezi 6 ambao wote umauti uliwakuta baada ya kushambuliwa na wahalifu wakiwa wamelala usiku. Katika tukio hilo wahalifu walimuacha mtoto mmoja Janeth Masabile mwenye umri wa miaka 5 akiwa amelala ndani bila kumjeruhi, na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa waliohusika na tukio hilo. MWISHO.

Category

Show more

Comments - 0