Duration 1:9

KARIBU HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA (TANAPA)

139 watched
0
0
Published 19 Aug 2020

Tembelea Hifadhi za Taifa Tanzania, Leo Tuanze na Hifadhi ya Taifa Arusha, hifadhi hii ina mandhari nzuri sana, ikiwa ni pamoja na uwepo wa Mlima Meru, wanyama wa aina mbalimbali ikiwemo nyati,twiga na wengineo, ni moja kati ya Hifadhi zenye maporomoko mazuri sana ya maji, unaweza kupanda mlima, kufanya matembezi au utalii wa Kutumia gari, gharama zake kwa raia wa Afrika Mashariki ni Tsh 11,800 tu kwa mtu mzima,na mtoto kati ya miaka 5-15 analipia 2,360, Bila kusahau walio chini ya miaka mitano ni bure. Wanafunzi wote wa primary,secondary na High school watalipia 2,360 tu, na walio katika colleges na Vyuo watalipia Tsh 5,900 tu, hii ni kwa wale wanaokuja kishule na sio private. Kama utafanya matembezi ni Tsh 5,900 kwa watu wazima kuanzia miaka 16, na kwa watoto kuanzia miaka 12 ni Tsh 2,950, kwa saa moja hadi manne. Lakini pia kama kikundi mtalipia gharama ya askari ambayo ni Tsh 5,900. Gharama za gari kuingia Hifadhini zinatofautiana kulingana na uzito wa gari utakayokuja nayo,Kumbuka shirika halina magari ya Utalii. gari zote zenye kilo chini ya 2000 zinalipia Tsh 23,600 tu, na zenye uzito wa kuanzia 2001-3000 ni tsh 41,300 , gharama zinapanda uzito wa gari unapoongezeka. Tukumbuke pia Hatupokei fedha taslim katika mageti (cash) , weka pesa yako katika kadi yako ya bank, tembo card,mastercard au visa card, Pia unaweza kuweka katika Mpesa,Tigo Pesa,Airtel Money na kuendelea ili utakapofika getini ufanye malipo ya serikali. Utalii wa ndani unaanza na Wewe. Malipo haya ya getini ni kwa wageni wanaojitegemea na sio wanaokuja na kampuni, kwani kampuni inalipia moja kwa moja katika mtandao uliopo kwenye tovuti yetu. #tanzaniparks #arusha #utaliiwandani

Category

Show more

Comments - 0